TECNO Phantom 8: Maelezo.

   

 

 Kwa wale wapenzi wa simu za TECNO hii ni mpya kutoka kwa kampuni hii. TECNO Phantom 8 imetoka kwenye msururu wa simu za TECNO Phantom ambako kumetokea simu kama TECNO Phantom 6 na 6 plus.

Kwa ujumla tu simu hii ya TECNO phantom 8 inatumia mfumo endeshi wa Android Nougat 7.0. inatumia kadi za sim mbili na iko na kioo cha inchi 5.7 ikiwa pia na 1080x1920 ambayo ni kiwango cha pixel 403 kwa kila inchi. Simu hii pia iko na uwezo wa kusevu hadi 64GB ambayo inaweza kuongezwa hadi 2TB na RAM ya 6GB ikiwa ni simu ya kwanza ya Tecno kuwa na RAM ya kiasi hicho. Betri ya simu hii inatazamiwa kuwa ya kiwango cha 3500mAh.

Sehemu Muhimu.

  • Mfumo endeshi: Android 7.0 Nougat na HiOS 3.0
  • kadi : Mbili (Micro)
  • 4G LTE: Ndio, LTE
  • Saizi ya Skrini : inchi 5.7
  • Resolusheni ya Skrini: 1080 x 1920 pixel (403 PPI)
  • Procesa: Octa-core 2.60 GHz Cortex, Mediatek chipset
  • RAM: 6GB
  • Memori ya ndani: 64GB.
  • Memori ya kuongeza: microSD, hadi 2TB
  • Kamera ya nyuma: 12MP + 13MP na LED Flashi
  • Kamera ya mbele: 20MP na LED flash
  • Betri: 3500 mAh

TECNO Phantom 8 inauzwa kwa bei ya Kshs.36 999 na pia iko kwa ofa ya muda mfupi ya hadi Kshs. 31 999 kwenye maduka ya jumia.

Comments

Popular posts from this blog

Whatsapp inakula memori yako?

INFINIX NOTE 5 IMEZINDULIWA!!

Google Pixel 2 na Pixel 2 XL