Whatsapp inakula memori yako?
Baada ya facebook kuchukua Whatsapp imeweza kuwa na watumiaji wa app hiyo zaidi ya bilioni moja dunia nzima. Wakati mwingi watumiaji wamekuwa na shida ya memori za simu zao kuisha bila wao kujua wafanyeje kujiokoa na shida hiyo.
Whatsapp imekuwa ikifungua picha va video bila hata ya kuamrishwa na hii ndio hufanya memori za simu kujaa bila ya mwenye simu kujua. Mbali na kujaza memori ya simu hii hali ya picha, video na audio kujidowload pia hula ile data utakuwa umeweka kwa simu hivyo basi kukufanya kuishiwa bundle za data kila wakati.
Leo tutawaonyesha jinsi ya kutatua shida hiyo.
Kwa simu za Androidi:
Kama wewe ni mtumiaji wa Androidi, fungua WhatsApp yako, nenda kwa Settings>Data and storage usage>Media auto download. Sasa toa tiki kwa boxi zote tatu kwenye Media auto download- when on mobile data, when connected on Wifi and when roaming.Kwenye iPhones:
Watumiaji wa iPhone pia wanaweza kufanya hivi. Fungua WhatsApp>Settings>Data and storage usage.Alafu tiki hiyo Never box ya photos, videos, audio na documents.
Low data usage for WhatsApp calls
WhatsApp pia iko na opsheni ya kupunguza kiwango cha data ya simu inayotumika wakati wa WhatsApp voice calls. Fungua WhatsApp>Settings>Data and storage usage> Low data usage.
Hii ndiyo jinsi ya kutatua matatizo haya.

Comments
Post a Comment