Google Pixel 2 na Pixel 2 XL

       Je Google itaweza kuiendesha biashara ya kutengeneza simu pamoja na kuwa kampuni ya kutengeneza mfumo endeshaji wa androidi? basi kwa kipindi cha mwaka mmoja google imeweza kutengeneza simu zinazoitwa pixel. Kwa saa hii Google imekuja na simu aina mbili Pixel 2 na Pixel 2 XL. Kama Google itaweza kupata mafanikio kwenye biashara ya utengezaji wa simu basi mauzo ya hizi simu mbili zinafaa kuwa juu ili kupea kampuni hii nafasi katika watengezaji simu mashuhuri duniani.
Simu za Google kawaida huja na mfumo endeshaji mpya au ule umetolewa na Google tu karibuni. Simu hizi mbili zinakuja na mfumo endeshaji 8.0 wa Oreo. Mfumo endeshaji wa Oreo unatumainiwa kuwa mfumo endeshaji wa simu bora sana duniani kwani hata ukitaka kuanzisha Google assistant ni rahisi tu sababu unaweza kuibofya simu na Google assistant itaanza.

Viungo muhimu vya simu hizi ni:

Pixel 2.

Uzito gramu 143

kioo 5'
Qualcomm Snapdragon 835 chipset
1980x1080 Resolution (441ppi)
Betri 2700mAh
Kamera ya nyuma 12MP
Kamera ya Mbele 8MP
Android 8.0
4 GB RAM na 64/128GB memory ya ndani


Pixel 2 XL

Uzito gramu 175
Kioo 6'
Qualcomm Snapdragon 835 chipset
2880x1440 Resolution (538 ppi)
Betri 3520mAh
Kamera ya nyuma 12.2MP f/1.8
Kamera ya Mbele 8MP
Android 8.0
4 GB RAM na 64/128GB memory ya ndani

Comments

Popular posts from this blog

Whatsapp inakula memori yako?

INFINIX NOTE 5 IMEZINDULIWA!!