Minong'ono ya Infinix Zero 5

       Kwa muda mwingi kampuni ya Infinix imejaribu kutengeza simu ambazo zingepigania mauzo ya simu pamoja na makampuni yaliyojistawisha kama apple na samsung. Katika wale watumiaji wa simu wenye kipato cha chini na wanahitaji kutumia simu za kisasa Infinix imeweza kuwatengenezea simu zinazoweza kufanya kazi sawa na za makampuni makubwa ya simu. Kwa wapenzi wa simu za Infinix kampuni hii inasemekana italeta simu mpya ya Infinix zero 5.
Simu hii inatazamiwa kuwa na mfumo endeshaji wa Android 7.0 Nougat na kupelekwa na prosesa ya 2.3GHz Octa-core. Kwa upande wa kioo, Infinix Zero 5 Plus itakuwa na skrini ya inchi 6 na pia  resolusheni ya 1920 x 1080.
Inasemekana pia itakuwa na RAM ya 6GB na 64GB memory ya ndani.
Katika sehemu ya upigaji picha, kamera ya nyuma ya 12MP ikiwa na auto-focus inatazamiwa na 5MP kwa kamera ya mbele ya picha za kupiga binafsi.
      

infinix zero 5 - infinix zero 5 plus

Zifuatazo ndizo sehemu za simu zinazodaiwa kuwepo kwa simu hiyo.

Infinix Zero 5 na Zero 5 Plus (X603)

Mfumo endeshaji:Android 7.0 Nougat Prosesa:2.0GHz octa-core
NetwakiGSM/WCDMA/LTE
Kioo:5.5″ SUPER AMOLED Touchscreen
Resolusheni:1920*1080
Kamera:16 MP kamera ya mbele yenye Wide-Angle Lens
16 MP AF Kamera ya nyuma
Memori:64GB ROM + 4GB RAM
  Inaezaongezwa na Micro SD, hadi 128 GB
Konektiviti:Wi-Fi, BT, GPS, USB Type C
SensaG-sensor, Light Sensor, Proximity Sensor, Hall sensor, Ecompass
Betri:3500mAh

Comments

Popular posts from this blog

Whatsapp inakula memori yako?

INFINIX NOTE 5 IMEZINDULIWA!!

Google Pixel 2 na Pixel 2 XL