Posts

Showing posts from November, 2017

TECNO Phantom 8: Maelezo.

Image
        Kwa wale wapenzi wa simu za TECNO hii ni mpya kutoka kwa kampuni hii. TECNO Phantom 8 imetoka kwenye msururu wa simu za TECNO Phantom ambako kumetokea simu kama TECNO Phantom 6 na 6 plus. Kwa ujumla tu simu hii ya TECNO phantom 8 inatumia mfumo endeshi wa Android Nougat 7.0. inatumia kadi za sim mbili na iko na kioo cha inchi 5.7 ikiwa pia na 1080x1920 ambayo ni kiwango cha pixel 403 kwa kila inchi. Simu hii pia iko na uwezo wa kusevu hadi 64GB ambayo inaweza kuongezwa hadi 2TB na RAM ya 6GB ikiwa ni simu ya kwanza ya Tecno kuwa na RAM ya kiasi hicho. Betri ya simu hii inatazamiwa kuwa ya kiwango cha 3500mAh. Sehemu Muhimu. Mfumo endeshi: Android 7.0 Nougat na HiOS 3.0 kadi : Mbili (Micro) 4G LTE: Ndio, LTE Saizi ya Skrini : inchi 5.7 Resolusheni ya Skrini: 1080 x 1920 pixel (403 PPI) Procesa: Octa-core 2.60 GHz Cortex, Mediatek chipset RAM: 6GB Memori ya ndani: 64GB. Memori ya kuongeza: microSD, hadi 2TB Kamera ya nyuma: 12MP...

Whatsapp inakula memori yako?

Image
Baada ya facebook kuchukua Whatsapp imeweza kuwa na watumiaji wa app hiyo zaidi ya bilioni moja dunia nzima. Wakati mwingi watumiaji wamekuwa na shida ya memori za simu zao kuisha bila wao kujua wafanyeje kujiokoa na shida hiyo. Whatsapp imekuwa ikifungua picha va video bila hata ya kuamrishwa na hii ndio hufanya memori za simu kujaa bila ya mwenye simu kujua. Mbali na kujaza memori ya simu hii hali ya picha, video na audio kujidowload pia hula ile data utakuwa umeweka kwa simu hivyo basi kukufanya kuishiwa bundle za data kila wakati. Leo tutawaonyesha jinsi ya kutatua shida hiyo. Kwa simu za Androidi: Kama wewe ni mtumiaji wa Androidi, fungua WhatsApp yako, nenda kwa Settings>Data and storage usage>Media auto download. Sasa toa tiki kwa boxi zote tatu kwenye Media auto download- when on mobile data, when connected on Wifi and when roaming. Kwenye iPhones: Watumiaji wa iPhone pia wanaweza kufanya hivi.  Fungua WhatsApp>Settings>Data and storage usage...

Minong'ono ya Infinix Zero 5

Image
       Kwa muda mwingi kampuni ya Infinix imejaribu kutengeza simu ambazo zingepigania mauzo ya simu pamoja na makampuni yaliyojistawisha kama apple na samsung. Katika wale watumiaji wa simu wenye kipato cha chini na wanahitaji kutumia simu za kisasa Infinix imeweza kuwatengenezea simu zinazoweza kufanya kazi sawa na za makampuni makubwa ya simu. Kwa wapenzi wa simu za Infinix kampuni hii inasemekana italeta simu mpya ya Infinix zero 5. Simu hii inatazamiwa kuwa na mfumo endeshaji wa Android 7.0 Nougat na kupelekwa na prosesa ya 2.3GHz Octa-core. Kwa upande wa kioo, Infinix Zero 5 Plus itakuwa na skrini ya inchi 6 na pia  resolusheni ya 1920 x 1080. Inasemekana pia itakuwa na RAM ya 6GB na 64GB memory ya ndani. Katika sehemu ya upigaji picha, kamera ya nyuma ya 12MP ikiwa na auto-focus inatazamiwa na 5MP kwa kamera ya mbele ya picha za kupiga binafsi.        Zifuatazo ndizo sehemu za simu zinazodaiwa kuwep...

Google Pixel 2 na Pixel 2 XL

Image
       Je Google itaweza kuiendesha biashara ya kutengeneza simu pamoja na kuwa kampuni ya kutengeneza mfumo endeshaji wa androidi? basi kwa kipindi cha mwaka mmoja google imeweza kutengeneza simu zinazoitwa pixel. Kwa saa hii Google imekuja na simu aina mbili Pixel 2 na Pixel 2 XL. Kama Google itaweza kupata mafanikio kwenye biashara ya utengezaji wa simu basi mauzo ya hizi simu mbili zinafaa kuwa juu ili kupea kampuni hii nafasi katika watengezaji simu mashuhuri duniani. Simu za Google kawaida huja na mfumo endeshaji mpya au ule umetolewa na Google tu karibuni. Simu hizi mbili zinakuja na mfumo endeshaji 8.0 wa Oreo. Mfumo endeshaji wa Oreo unatumainiwa kuwa mfumo endeshaji wa simu bora sana duniani kwani hata ukitaka kuanzisha Google assistant ni rahisi tu sababu unaweza kuibofya simu na Google assistant itaanza. Viungo muhimu vya simu hizi ni: Pixel 2. Uzito gramu 143 kioo 5' Qualcomm Snapdragon 835 chipset 1980x1080 Resolution (441ppi) Be...