HUAWEI Y7 PRIME (2018)
Baada ya kuja na simu ya Huawei Y7 prime ya mwaka 2017 kampuni ya kutoka China ya Huawei imetoa simu nyingine ya mtindo huo huo lakini wakaiboresha. Kwa wale wapenzi wa simu za budget yaani bei zisizoumia mfuko wako kwa sana wanaweza kununua simu hii kutoka kwa website ya kilimall ambao wanashirikiana na kampuni ya Huawei kuuza bidhaa hii nchini Kenya. Maelezo ya simu hii kwa ufupi: Mfumo endeshi: Android version 8.0 Oreo RAM: 3 GB ROM: 32 GB Kamera: Nyuma 13MP + 2MP Mbele 8 MP Saizi: inchi 5.99 Prosesa: 1.4 GHz Octa Core Cortex-A53 Rangi: Nyeusi, Dhahabu na Samawati Iko na uwezo wa 4G LTE Uzito: 155 gramu Vipimo vyake ni: 158.3 x 76.7 x 7.8 mm Betri : 3000 mAh Hivi ndivyo simu hii inakaa kwa picha Inapatikana kwa preorder kwenye twavuti ya kilimall .